UNCDF yakwamua wakulima wa muhogo nchini Tanzania by UN News Kiswahili published on 2016-03-23T17:43:12Z Nchini Tanzania, Umoja wa Mataifa kupitia mfuko wake wa maendeleo ya mitaji, UNCDF unasaidia kukwamua harakati za sekta binafsi na ile ya umma katika kusongesha maendeleo ya wananchi mashinani. Miongoni mwa harakati hizo ni hatua ya hivi karibuni zaidi ya kusaidia kuinua wakulima wa zao la Muhogo katika wilaya ya Rufiji, mkoa wa Pwani kwa kusaidia kiwanda cha African Starch Company. Assumpta Massoi anasimulia zaidi katika makala hii iliyowezeshwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.