MAKALA- Akipata mimba utotoni, kuna uwezekano mtoto wake hatosoma by UN News Kiswahili published on 2021-06-09T16:23:43Z Umoja wa Mataifa kupitia malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, unahamasisha kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, usawa wa kijinsia na mengine kama hayo ambayo kwa pamoja yanamhakikishia mwanadamu ustawi bora wa maisha yake. Nchini Tanzania, wadau mbalimbali wa elimu na masuala ya watoto hususani wa kike, wamekuwa wakipaza sauti za kutaka kubadilishwa kwa sera zinazowazuia watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni, kuzuiliwa kuendelea na masomo yao. John Kabambala wa redio washirika KidsTime FM ya Morogoro Tanzania ameliangazia suala hilo ambalo linaanza kupata nuru kutokana na kauli ya waziri wa elimu wa nchi hiyo. Genre News & Politics