Kilimo hai sio tu kinalinda mazingira lakini pia afya za watu:Kitojo 16-09-2021 by UN News Kiswahili published on 2021-09-16T20:11:29Z Kilimo hai kina mchango mkubwa katika kutimiza ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa SDG’’s hasa katika kulinda mazingira, kuhakikisha uhakika wa chakula na pia kutimiza moja ya vipengele vya lengo la afya bora. Kwa mujibu wa Bwana Waziri Kitojo, Afisa Kilimo wa kampuni ya kilimo ya Digital Mobile Africa ya nchini Tanzania kilimo hai licha ya kusaidia kupambana na uhariubifu wa mazingira kinafaida kiafya kwani chakula kinachozalishwa hakitumii kemikali bali mbolea za asili kama samadi na mboji. Kupata ufafanuzi zaidi wa kilimo hicho na faida zake Anold Kayanda amezungumza na Bwana Kitojo ambaye anaanza kwa kueleza maana ya Kilimo Hai. Genre News & Politics