Jaridani na Assumpta Massoi 14-06-2021 by UN News Kiswahili published on 2021-06-14T15:14:31Z Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea -Leo ni siku ya uchangiaji damu duniani shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO likisema inajikita na mchango wa vijana katika uchangiaji wa damu -Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM linamuombeleza aliyewahi kuwa mkurugenzi wake mkuu William Lacy-Swing aliyeaga dunia mwishoni mwa wiki -Shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO kesho litazindua ripoti kuhusu wafanyakazi wa majumbani kutathini hali tangu kupitishwa mkataba na athari za COVID-19 kwa wafanyakazi hao -Mada kwa kila leo inajikita la lengo la maendeleo endelevu namba 7 au SDG-7 likijikita na nishati jadidifu nchini Tanzania -Na mashinani tuko New york utamsikia mkulima anayetaka kijani kitapakae na pia ni mpishi wa chakula anachopanda Genre News & Politics