Jarida 06 Julai 2022 na Assumpta Massoi - Maadhimisho ya Kiswahili UN na Jumuiya ya Afrika Mashariki by UN News Kiswahili published on 2022-07-06T15:05:27Z Hii leo jaridani ni mada kwa kina tukiendelea kupazia siku ya kiswahili duniani na leo Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Profesa Kennedy Gastorn anaelezea kile watakachofanya kesho hapa Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani. Halikadhalika Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki anaelezea shamrashamra huko Zanzibar, Tanzania .Mashinani ni harakati za kusongesha kiswahili Burundi na usisahau leo kuna Habari kwa Ufupi zikiletwa na Anold Kayanda akimulika ripoti ya hali ya njaa duniani, SOFI, hali ya upatikanaji wa chakula Sri Lanka halikadhalika salamu za rambirambi za Katibu Mkuu wa UN kufuatia shambulio dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Mali. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi. Genre News & Politics